China yaipiku Marekani kwa kompyuta bora

Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa hivi karibuni zaidi, China ina kompyuta bora na yenye nguvu zaidi duniani inayojulikana kama 93 petaflop Sunway TaihuLight, ambayo imeshinda zile zilizokuwa zikisifika huko nyuma zilizobuniwa Marekani. Orodha hiyo inaonesha kuwa kompyuta ya TaihuLight imewekwa katika ofisi za National Supercomputing, iliyoko Wuxi, katika kilele chake, kompyuta hii anaweza kufanya karibu mahesabu trilioni China yaipiku Marekani kwa kompyuta bora 93,000 kwa sekunde. Kompyuta hiyo ina kasi mara mbili zaidi ya ile iliyokuwa

 

ikiongoza ya Tianhe-2, pia kutoka China, jarida la Top500 linasema. Weledi wa Kompyuta hii upo katika sekta ya uzalishaji, utabiri wa hali ya anga, tathmini ya data kubwa za mashirika kwa mujibu wa mtafiti Jack Dongarra. Mashine hii ina zaidi ya 'Nodes' 40,960 huku ikitumia mtambo wa programu maarufu ya Linux. Kwa mara ya kwanza tangu orodha hii ianze, China imeipiku Marekani ikiwa na kompyuta 167 katika ya 500 bora. Marekani ina 165. Marekani ina kompyuta nne kati ya 10 bora katika orodha hiyo ya Top500, wakati China ina mbili ambazo kwa sasa

zinachukua nafasi ya kwanza na ya pili. Nafasi zingine katika kumi bora zinachukuliwa na mashine kutoka Japan, Uswisi, Ujerumani na Saudi Arabia.