ISRAELI

Price:Tsh. 8,000


Author: Rev. E. S. Munisi


Publisher / Printer : NIIM COMPUTERS


Dar es Salaam, Tanzania


Edition:

Ni taifa lililopigana vita tangu mwanzo wa kuzaliwa kwake likiwa na baba yao Yakobo ambaye ndiye Israeli miaka zaidi ya elfu tatu iliyopita hadi leo. Lakini pia ndilo taifa lenye mchango mkubwa zaid ya yote kwenye ustaarabu na maendeleo ya dunia. Na ijapokuwa ni taifa dogo sana, limejulikana kuwa na uwezo mkubwa wa kijeshi na mbinu za kivita zinazoushangaza ulimwengu.

Huu upekee wa taifa hili unatokana na nini? Au ni bahati tu? Sio bahati tu. Taifa hili ni taifa teule la Mungu kama Biblia isemavyo. Kwa kupitia taifa hili Mungu alikusudia kuupata tena ulimwengu uliopotea kwa njia ya Masihi aliyekuja kwa njia ya taifa hilo

Mambo matukufu sana yametokea kwenye taifa hili. Maandiko Matakatifu yanayoaminika kuwa ndiyo pekee yaliyotoka kwa Mungu yametokana na watu wake. Masihi aliye pekee Mwokozi wa ulimwengu ametokana na taifa hili. Na utimizo wa unabii wa siku za mwisho unahusiana kwa asilimia mia moja na taifa hili. Ndilo ishara kuu ya kinabii katika Biblia.

Kulielewa vyema taifa hili na jinsi linavyohusiana na mpango wa Mungu wa kinabii ni lazima kwa mwanafunzi wa unabii kuelewa somo hilo muhimu. Kitabu hiki kinachambua kwa kina upekee wa taifa hili kuhusiana na utimizo wa unabii wa siku za mwisho. Kisome kwa moyo wa kujifunza, nawe utatajirishwa na Roho wa Bwana kipekee.